¡Acompáñanos a viajar por el mundo de los libros!
Añadir este libro a la estantería
Grey
Escribe un nuevo comentario Default profile 50px
Grey
Suscríbete para leer el libro completo o lee las primeras páginas gratis.
All characters reduced
Hadithi Yako ya Kweli - Mwongozo Muhimu wa Siku 50 Kwa Ajili ya Maisha Yako Mapya Pamoja na Yesu - cover

Hadithi Yako ya Kweli - Mwongozo Muhimu wa Siku 50 Kwa Ajili ya Maisha Yako Mapya Pamoja na Yesu

Susan Freese

Traductor Lingua Christian

Editorial: Publishdrive

  • 0
  • 0
  • 0

Sinopsis

JINUNULIE KIMOJA. MNUNULIE MTU KIMOJA KAMA ZAWADI.* Maisha yako yanaweza kubadilika ndani ya Siku 50. Zana hii KAMILI ya Kujifunza Biblia ina mambo muhimu juu ya uanafunzi kwa ajili ya Wakristo wapya ulimwenguni kote (hakuna mifano ya kimagharibi). Ni vigumu kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu na kutimiza kusudi lako bila ufahamu mzuri wa hadithi Yake na sehemu yako katika hadithi hiyo.
 
Masomo haya 50 ya kila siku yanafunua MAMBO MUHIMU YA IMANI ili kufanya urafiki wako na Yesu uwe wa kina na kukupa UJUZI WA KIUTENDAJI ili iwe mfuasi Wake.
 
Jifunze kile ambacho waumini wakomavu wamejua kwa miaka mingi ndani ya Siku 50 kupitia safari hii rahisi lakini inayobadilisha maisha.
 
Wiki ya 1:    Hadithi ya Mungu—Kugundua hadithi kuu ya Biblia
 
Wiki ya 2:    Hadithi Yako—Kukumbatia utambulisho wako mpya katika Kristo
 
Wiki ya 3:    Kusudi Lako—Kutimiza kusudi la maisha yako
 
Wiki ya 4:    Kukaa Ndani—Kubaki Ukiwa Umeunganishwa  na Mungu
 
Wiki ya 5:    Neno la Mungu—Kumsikiliza Mwanzilishi wa Uzima
 
Wiki ya 6:    Neno la Mungu—Kunena na Mwanzilishi wa Uzima
 
Wiki ya 7:    Roho Mtakatifu—Kutimiza Hadithi Yako Kwa Nguvu Za Mungu
 
Kila wiki utajifunza zaidi juu ya simulizi ya Biblia.
 
Utagundua siri za maisha ya Kikristo, kama vile jinsi ya kukaa ndani ya Kristo, kushughulikia shaka, kupinga majaribu, na kumwabudu Mungu katika misimu ya mateso.
 
Pia utajifunza njia za kiutendaji za kujifunza Biblia yako, kushiriki imani yako, kufanya wanafunzi, na kuomba. Ikiwa hujaanzisha uhusiano na Yesu, utapata fursa ya kuchukua hatua hiyo.
 
Kila siku inatamatishwa kwa mbinu ya Amri Kuu ya kutumia Maandiko, maswali, maombi, na mahali pa kuchukua hatua zako zinazofuata.
 
KITABU HIKI NI KWA AJILI YAKO IKIWA:
 
- Wewe ni muumini mpya katika Yesu unayetafuta hatua zinazofuata za kukuza imani yako,
 
- Wewe ni Mkristo anayetafuta kufundishwa kuwa mwanafunzi au kuwafundisha wengine kuwa wanafunzi,
 
- Unachunguza Ukristo na unataka kujua jinsi ya kuwa mfuasi wa Yesu.
 
MAISHA YAKO YANA HADITHI MPYA YA KUSIMULIA:
 
Shuhudia imani ya kweli na furaha unapotumia kweli takatifu kubadilisha maisha yako. Kukutana na Yesu ni mwanzo tu. Kumfuata--hivyo ndivyo hadithi yako ya kweli inavyojitokeza.
 
--Maneno muhimu, maswali ya kutafakari ya kibinafsi ya kila siku na ya majadiliano ya kikundi ya kila wiki yamejumuishwa.
 
-- Kimeandikwa kwa ajili ya wasomaji kutoka kote duniani bila mifano ya kimagharibi.
 
--Zaidi ya saa 10,000 za utafiti, hakiki 3 za kitheolojia, marejeo zaidi ya 1,400 ya kibiblia, wasomaji zaidi ya 50 wa kutoa maoni ya awali = Safari 1 Inayobadilisha Maisha.
 
Taarifa zaidi zinapatikana kwenye yourtruestorybook.com
 
Mapato kutoka kwa kila kitabu kinachouzwa yatatoa nakala iliyotafsiriwa kwa muumini ambaye hana nyenzo za kutosha katika nchi inayoendelea.
Disponible desde: 19/01/2024.
Longitud de impresión: 368 páginas.

Otros libros que te pueden interesar

  • japji kiswahili kutafakari - safari kwa roho - cover

    japji kiswahili kutafakari -...

    Thaminder Singh Anand

    • 0
    • 0
    • 0
    1.safari kwa roho 
    2.Safari ya kuelekea Kiroho 
    Guru Granth Sahib ni Guru aliye hai wa milele, muundo wa kishairi wa Sikh Gurus, Watakatifu wa Kihindu na Waislamu. Mkusanyiko huo ni zawadi kutoka kwa Mungu kupitia kwao kwa wanadamu wote. Maono katika Guru Granth Sahib ni ya jamii yenye msingi wa haki ya Kimungu bila ukandamizaji wa aina yoyote. Ingawa Granth inakubali na kuheshimu maandiko ya Uhindu na Uislamu, haimaanishi upatanisho wa maadili na mojawapo ya dini hizi. Katika Guru Granth Sahib wanawake wanaheshimiwa sana na majukumu sawa kama wanaume. 
    Wanawake wana roho sawa na wanaume na hivyo wana haki sawa ya kukuza hali yao ya kiroho na nafasi sawa ya kupata ukombozi. Wanawake wanaweza kushiriki katika shughuli zote za kidini, kitamaduni, kijamii, na kidunia ikiwa ni pamoja na kuongoza makutano ya kidini. Sikhism inatetea usawa, haki ya kijamii, huduma kwa ubinadamu, na uvumilivu kwa dini zingine. Ujumbe muhimu wa Kalasinga ni ibada ya kiroho na uchaji wa Mungu wakati wote wakati wa kutekeleza maadili ya huruma, uaminifu, unyenyekevu na ukarimu katika maisha ya kila siku. Kanuni tatu za msingi za dini ya Sikh ni kutafakari na kumkumbuka Mungu, Kufanya Kazi kwa ajili ya kuishi kwa Uaminifu na kushiriki na wengine.
    Ver libro
  • Mungu wa Ajabu - cover

    Mungu wa Ajabu

    André Cronje

    • 0
    • 0
    • 0
    Mungu wa Ajabu: Ni utukufu wa wafalme kutafuta siri za dunia na kupata siri za ufalme wa Mungu. Dunia yote imejaa utukufu wake, na viumbe vyote vinapaaza sauti vikitaja jina lake kwa sifa na kuabudu. Mungu wa Ajabu imejaa mashairi na sifa ili kuhamasisha imani yako na mkusanyiko wa mawazo. Kama vile mtunga-zaburi alivyosema, ulimi wangu ni ule wa mwandishi aliye tayari kumpa ukuu mfalme wangu.
    Ver libro
  • The Glorious Arrest of a Family - SWAHILI EDITION - School of the Holy Spirit Series 8 of 12 Stage 1 of 3 - cover

    The Glorious Arrest of a Family...

    Lambert Okafor

    • 0
    • 0
    • 0
    Kukamatwa kwa Utukufu wa Familia
    
    Uwepo wa Mungu ulionekana mbele yao nyumbani kwao na ulidumu kwa siku tatu. Kufikia siku ya tatu Mungu alikuwa amebadilisha maisha ya wote katika familia, kutia ndani yale ya mgeni! Aliwaonyesha mafumbo makubwa na matukio ambayo yangetokea hivi karibuni ulimwenguni; Kisha akawauliza “nendeni mkawaambie kila mtu” yale waliyoyaona. Kabla ya tukio hili Bwana & Bibi Okafor walikuwa na wakati mdogo au hawakuwa na wakati wa mambo ya Mungu. Leo, hadithi ni tofauti. “Mwisho wa mambo yote umefika na lazima tusaidie kuwaonya wananchi” mwandishi anasema.
    "...Ujumbe huu ni wa kuvutia, wa upendo, chini kabisa na ni wa HARAKA... Napendekeza kitabu hiki kwako ukisome na...kwa kuchukua hatua zinazofaa."
    Ver libro
  • How To Hear From God - SWAHILI EDITION - School of the Holy Spirit Series 7 of 12 Stage 1 of 3 - cover

    How To Hear From God - SWAHILI...

    Lambert Okafor

    • 0
    • 0
    • 0
    NAMNA YA KUSIKIA KUTOKA KWA MUNGU
    Niliandika kijitabu hiki kwa sababu ya maswali mengi niliyopokea kutoka kwa waamini, wengine kupitia barua na wengine kupitia ziara za kibinafsi, yote yakihusu jinsi ya kusikia kutoka kwa Mungu! Nilishangaa mara ya kwanza wakati baadhi ya maswali yalipotoka kwa watu niliowaona kuwa Wakristo waliokomaa sana. Punde, niligundua kwamba hili lilikuwa tatizo moja ambalo kwa hakika lilikumba kada zote za waumini, lakini tatizo moja ambalo lilizingatiwa mara chache sana katika makanisa yetu mbalimbali!
    Si ajabu watu wanaona ni rahisi kusema, “mchungaji wangu alisema…”, badala ya “Bwana alisema”! Na kwa hivyo, wakati mchungaji anapoteleza, kila mmoja pia anajitenga naye, kwa sababu hakuna anayeweza kufanya uchunguzi wa kujitegemea moja kwa moja kutoka kwa Bwana. Hiyo ni sawa na Waisraeli kule Jangwani ambao waliweza tu kusikia na kumnukuu Musa, lakini hawakuthubutu kuingiliana na Mungu wao moja kwa moja. Katika mchakato huo, wote waliangamia kwa kuwa hawakujua njia za Mungu! Ni jambo la hatari kama nini wakati huu wa mwisho kwa mwamini yeyote kumtegemea kabisa mchungaji!
    Iliuumiza moyo wangu zaidi nilipogundua kwamba Bwana alikuwa akizungumza na wengi wa watu hawa, tu kwamba, kama Samweli, hawakuweza kutambua sauti yake. Walichohitaji tu ni mtu wa kuwaelekeza, kama vile Eli alivyomfanyia Samweli. Na akina Eli wa wakati wetu wanaonekana kuwa na shughuli nyingi sana na masuala mengine.
    Ikiwa wewe ni mmoja wa wale ambao wamekuwa wakiteseka kimya kwa muda mrefu juu ya suala hili la kusikia kutoka kwa Baba yako wa Mbinguni, unapaswa sasa kufurahi kwa kuwa hitaji lako litatimizwa hivi karibuni, na Bwana Mwenyewe, kupitia mikataba hii ndogo.
    
    Bwana Yesu akubariki sana unaposoma. Amina.
    
    Lambert .E. Okafor
    Ver libro
  • Sauti Ya Mungu Yenye Nguvu - cover

    Sauti Ya Mungu Yenye Nguvu

    Rev. Robert A. Tucker

    • 0
    • 0
    • 0
    Mara nyingi, Wakristo wengi hawaitambui sauti ya Mungu au hudanganyika kufikiri kwamba sauti nyingine ni sauti ya Mungu. Mchungaji Tucker atawatia moyo wasomaji kwamba kwa kweli wanaweza kuisikia sauti ya Mungu kibinafsi. Atayajibu maswali haya:
    
    	Jinsi gani tunaweza kuijua sauti ya Mungu?
    	Jinsi gani tunaweza kuitofautisha sauti ya Mungu na sauti nyingine nyingi duniani?
    	Jinsi gani tunaweza kuepukana na udanganyifu?
    	Kuna uhusiano gani kati ya kuisikia sauti Yake na imani, haki na hekima?
    Ver libro
  • 4 – Hour Interviews in Hell - SWAHILI EDITION - School of the Holy Spirit Series 12 of 12 Stage 1 of 3 - cover

    4 – Hour Interviews in Hell -...

    Yemi Bankole

    • 0
    • 0
    • 0
    4 - Mahojiano ya Saa huko Kuzimu
    
    Huu ni ujumbe kutoka nchi ya mbali. Imekusudiwa kwa ulimwengu; kusomwa na mamilioni; kuaminiwa na wanyenyekevu; iliyoombewa na wenye hekima. Ingawa, bahari itavukwa na kisiwa kuchunguzwa; ijapokuwa maarifa yataongezeka na hekima itatengeneza piramidi, lakini kila nafsi itaishi kuliko jua, na roho ya mwanadamu haitasafiri kuingia.
    kutoweka. Katika nchi, katika mwaka, katika siku katika mahali, mwili na roho vitatengana. Hakuna malalamiko, hakuna kisingizio, hakuna rufaa, hakuna mwanasheria, wakati roho zetu zitajibu nyumbani - wito wa Mungu. Uzuri kwa nchi mbaya, ulio juu kwa mavumbi chini, mavumbi hurudi mavumbini, lakini roho huruka mbali. Tamthilia ya mwisho ni ya marehemu kukaa kimya kana kwamba yu hai chini ya neno "Mazishi" na kuheshimiwa kwa '''Marehemu' jina la herufi 4 linalofuata jina lake kwa umilele uliobaki, kumwambia kila mtu anayeweza kusoma. kwamba hapo zamani alikuwa mkaaji wa nchi hii yenye viraka. Sisi ni dhaifu na mdogo. Sisi sote ni ndege wa kupita. Tumepewa lakini kwa utukufu wa muda mfupi.
    Msomaji wangu mnyenyekevu, inuka, jua linazama na giza linakuja, tumia fursa na uchukue fursa. Imekuwa dini wakati wote, sasa ni wakati wa wokovu wa kweli, sasa ni kufanya utakatifu kuwa mpigo wa moyo wako. Jiandikishe kwa ajili ya mbinguni wakati wokovu ni nafuu na roho yako iko tayari.
    Ver libro